
Thank you for reading this post, don’t forget to subscribe!Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi endapo atachaguliwa kuiongoza Tanzania, Serikali yake itaendelea kuvisimamia vyama vya ushirika ili kuhakikisha wakulima wanafaidika, sambamba na kuondoa ubadhilifu wa fedha za wana ushirika.
Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wananchi katika Mkutano wale wa Kampeni za CCM, uliofanyika leo Septemba 26,2025 kwenye viwanja vya Sabasaba Mkoani Mtwara.
Pamoja na ahadi hiyo, Dkt. Samia pia ameahidi Amesema kushughulikia ucheleweahwaji wa malipo kwa wakulima unaosababishwa na ubadhilifu ndani ya vyama vyao.
“Vyama vya ushirika tunavijenga ziwe taasisi zinazoweza kujitegemea katika uendeshaji wa kilimo chetu na kuwasaidia wakulima kuweza kueendesha shughuli zao” amesema Dkt. Samia.
Aidha Dkt. Samia ameeleza kuwa katika kipindi cha uongozi wake Serikali imeanzisha Benki ya ushirika ili kuweza kutoa huduma bora kwa vyama vya Ushirika.
Katika hotuba yake, Dkt. Samia pia ameeleza azma ya Serikali yake kuendelea kuyapima maeneo ya wafugaji, ambapo amesema endapo atapata ridhaa ataendelea kutafuta masoko kwa mazao yote yanayozalishwa nchini. na kuendelea kuvutia wawekezaji kwaajili ya ujenzi wa viwanda vya kuchakata korosho katika Kongani ya viwanda iliyopo katika kijiji cha Maranje Wilayani Mtwara
“Mkitupa ridhaa, tutaendelea kutafuta masoko ya uhakika, na sio tu kwa Korosho lakini kwa mazao yote tunayozalisha nchini ikiwemo ufuta na mbaazi, na tutaendelea kuvutia wawekezaji kwaajili ya ujenzi wa viwanda vya kuchakata korosho katika Kongani ya viwanda iliyopo pale kijiji cha Maranje katika Wilaya ya Mtwara” amesema Dkt. Samia.











