TUTAJENGA MTANDAO WA GESI KUTOKA KINYEREZI HADI CHALINZE – Dkt. SAMIA

0
16

Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kujenga mtandao wa gesi kutoka Kinyerezi hadi chalinze endapo atapata ridhaa kuongoza Serikali kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.

Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo alipowahutubia maelfu ya wananchi wa Kibaha, katika Kampeni za Chama hicho uliofanyika leo Septemba 28, 2025, Kibaha Pwani.

Amesema, ujenzi huo utakuwa na matoleo kuelekea kwenye maeneo ya uwekezaji ya TAMCO, Zegereni, Kwala na Bagamoyo ambapo kwa sasa mkabdarasi mshauri anaendelea na tathimini ya njia ya kupitisha Bomba la gesi.

“Ujio wa gesi utazidi kuvutia wawekezaji mkoani humu, naviwanda vitaweza kuendeshwa kwa gharama nafuu, na bidhaa zinazozalishwa zitapungua bei” amesema Dkt.Samia.

Aidha Dkt. Samia ameahidi kuendelea kuchukua hatua za kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi nchini ili kuwezesha wananchi hususani wa kipato cha chini kujenga nyumba bora na za kisasa kwa gharama nafuu.

“Mwelekeo wa serikali ni kuendeleza mpango wa ujenzi wa makazi bora kwa bei nafuu, na Mkoa wa Pwani umekuwa wa mfano katika kuibeba ajenda hii ya Kitaifa.

“Tutaendelea pia kuboresha makazi Mijini kwa kuhakikisha nyumba, makazi na majengo yote yanarasimishwa kwa kupimwa, kupangwa na kumilikishwa“Dkt. Samia Suluhu Hassan,

#mamakajatz

#Oktobatunatiki

#samiamitanotena

  

Author

  • Dawati Huru

    Dawati Huru Media ni jukwaa la habari za kitaita, kimataifa, biashara, utalii sanaa na michezo. Ni meza moja inayokuletea mkusanyiko wa kila unachohitaji katika tasnia hii.

    View all posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here