NHC KUIBADILISHA KARIKOO UTEKELEZAJI SERA YA UBIA

0
20

Kiwanja Na. 1/19 Uhuru/Congo – Hatua ya ujenzi ilipofikia.

 UTEKELEZAJI WA SERA YA UBIA

Baada ya sera mpya ya ubia iliyozinduliwa Novemba 16, 2022, Shirika la Nyumba la Taifa NHC lilitangaza maeneo kadhaa kwa ajili ya uwekezaji wa Sekta Binafsi. Januari 2024, Shirika liliidhinisha na kusaini mikataba ya miradi 20 ya ubia yenye thamani ya TZS 179 bilioni. Kwa sasa Miradi 18 tayari imekabidhiwa kwa Wabia kwa ajili ya kuanza ujenzi. Miradi tisa (9) ilikabidhiwa Februari 2024 na ujenzi wake tayari umeanza na ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi, mingine ikiwa imefikia hadi sakafu ya saba.

Aidha, Miradi nane (8) ilikabidhiwa kipindi cha Julai mpaka Agost 2024 na iko kwenye hatua mbalimbali za ujenzi, ikiwa ni kuchimba msingi na sakafu ya chini mpaka sakafu ya kwanza. Miradi miwili (2) imekabidhiwa Oktoba 2024 na iko kwenye hatua mbalimbali za maandalizi ya kuanza ujenzi (kuvunja majengo ya zamani, kukusanya vifaa vya ujenzi, kuchimba misingi, nk.). Kadhalika, Mradi mmoja (1) upo kwenye hatua ya kuomba vibali vya ujenzi na kukamilisha taratibu mbalimbali za mkataba.

Kiwanja Na. 9 &10/28 Uhuru/Swahili/Aggrey, hatua ya ujenzi ilipofikia sasa

  • Usimamizi wa Miradi ya Ubia

Shirika limeendelea kusimamia miradi ya ubia ya sasa na ya zamani iliyokuwa imesimama ambayo ipo maeneo mbalimbali nchini. Miradi minne iliyokuwa imesimama imesharejeshwa kwenye Shirika ili ikamilishwe na Shirika lenyewe. Lengo la Shirika ni kuhakikisha miradi yote ya ubia isiyokamilika inarejeshwa katika Shirika na mazungumzo na wabia wenye miradi hiyo yanaendelea.

Kadhalika, Shirika linaendelea na mchakato wa upembuzi na tathimini ya kina kwa waombaji wapya kwa miradi mingine kwenye maneneo yake kadhaa yanayohitaji kuendelezwa na sasa iko kwenye hatua ya kupata vibali kwa ajili ya  viwanja hivyo visivyopungua 80 kwa nchi nzima.

Kiwanja Na. 13 &14/6 Uhuru – Hatua ya ujenzi ilipofikia.

Author

  • Dawati Huru

    Dawati Huru Media ni jukwaa la habari za kitaita, kimataifa, biashara, utalii sanaa na michezo. Ni meza moja inayokuletea mkusanyiko wa kila unachohitaji katika tasnia hii.

    View all posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here